Unafahamu Kiswahili? Mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Idd Aziz kutoka
nchini Kenya ameachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Kiswahili.’ Ukihusu
lugha adhimu ya Kiswahili, wimbo huu maridhawa umedhamiriwa
kuwaunganisha wapenzi wa muziki na wajuzi wa lugha hiyo duniani kote.
Idd anauelezea KISWAHILI, “Nilitaka kutengeneza wimbo ambao hautaishia kuwa mzuri tu lakini pia uwe na ujumbe mkubwa utakaodumu kwa vizazi vingi. Nahisi
kuwa wanamuziki wa Kenya wakati mwingine huchukulia poa lugha za
nyumbani, hasa Kiswahili hivyo huu utatukumbusha maana mahsusi ya
Kiswahili na tafsiri yake ya pekee.”
Ukiandikiwa na kuimbwa na Idd Aziz, KISWAHILI umetayarishwa na Jesse wa Revive Media huku video yake ikiongozwa na Sync. Kwenye video yake, Idd anaigiza
kama mwalimu wa shule ya msingi huku hadithi yake ikitupeleka darasani
ambako kupitia wimbo, anawafundisha wanafunzi umuhimu wa kushika urithi
wetu kwa kujifunza Kiswahili.
Vitabu mashuhuri vya Kiswahili vya mtaala wa Kenya vinaonekana kwenye video hii iliyoongozwa kwa umahiri mkubwa.
KISWAHILI
ni wimbo halisi wa Kikenya wenye vionjo vya Afrika Mashariki. “ Wimbo
na ujumbe wa wimbo huu vimeshiba. Naamini mtaupenda. Nitaendelea kuachia
nyimbo nzuri za Kiswahili,” anasema Iddi.
USIKILIZE KISWAHILI kwenye Soundcloud: http://bit.ly/1O2zPok
IDD AZIZ - KISWAHILI (Official Music Video)
Reviewed by Admin
on
10:12:00 PM
Rating:
